Kampuni
ya Swissport inayojishughulisha na utoaji wa huduma katika viwanja vya ndege
nchini imeajiri vijana 178 kutoka vyuo mbalimbali vya VETA katika kipindi cha
miaka mitatu baada ya kubaini kuwa vijana hao wana ujuzi na uadilifu katika
kazi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Swissport nchini Mriso Bakari Yassin aliyabainisha hayo hivi
karibuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mjini ofisi
za Swissport katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Yasini
alisema kuwa kati ya vijana hao 150 wametoka chuo cha VETA Dar es Salaam na 28
wametoka chuo cha VETA Moshi.
“Kwa
sasa Swissport tunaamini zao la VETA ni zao bora kwa shughuli zetu na
tutaendelea kuwatumia wahitimu wa VETA kwa kadri tutakavyokuwa tunahitaji
wafanyakazi,” alisema.
Aliongeza
kuwa baada ya kujenga imani kubwa kwa VETA na vijana wake, kampuni yake
inafikiria kuingia makubaliano na VETA ili ikasimishe kwake kazi ya usafi
katika viwanja vya ndege inavyovihudumia, kwa kuwa inafundisha pia kozi ya
usafi.
Aliwashauri
waajiri wengine kuwaamini na kuwatumia vijana kutoka VETA kwani ni vijana
mahiri na waadilifu katika kazi.
No comments:
Post a Comment