Wasichana
nchini wameshauriwa kujiunga na kozi ya uendeshaji mitambo inayotolewa katika
chuo cha VETA Shinyanga ili kujipatia ajira kwa urahisi na kujikwamua kiuchumi kutokana
na fani hiyo kuwa na fursa nyingi katika
soko la ajira.
Akizungumza chuoni
hapo, Mkufunzi wa Uendeshaji mitambo mikubwa Aclay Fraten alisema mwitikio wa
wasichana kusoma kozi hiyo bado ni mdogo sana ukiliganisha na wavulana.
Kwa mujibu wa
Mwalimu Fraten kati ya wanafunzi 149 wanaosoma fani hiyo wasichana ni 11 tu na
kwamba changamoto inatokana na dhana iliyojengeka kuwa kazi za mitambo ni za wanaume pekee
“Imefikia
wakati wa kubadili mtizamo na kuona fani hiyo hata wasichana wanaweza na sio
kuwaachia wavulana tu.
Mmoja wa
mwanafunzi wa kozi ya Uendeshaji wa Mitambo kutoka mkoani Morogoro, Happiness
Msopola alisema alitamani kujua uendeshaji wa mitambo siku nyingi na kwamba ni
kozi anayoipenda kutoka moyoni, lakini hakuwa na taarifa kozi hiyo inapatikana
wapi hadi alipopata taarifa kuwa inapatikana
Chuo cha VETA Shinyanga.
Alisema kuwa
kozi hiyo ni rahisi tofauti na baadhi ya wasichana wengi wanavyodhani kuwa kozi hizo ni kwa wanaume
pekee“Tena naona
hii kozi inawafaa zaidi wanawake, maana hata uendeshaji wake si mgumu, kwa hiyo
nawashauri wanawake wenzangu wajifunze hii kozi ili tuweze kujikwamua na
maisha. ….. Ninawaomba waajiri watuamini, wasione tu kwamba pengine wanatuajiri
kwa kutusaidia kwa sababu ni wanawake. Watuajiri wakijua kuwa wanaajiri watu
mahiri na wanaojiweza.,” alisema.
Alisema wakati anaanza kusoma kozi hiyo hakuwa na uelewa wa kifaa chochote
katika mitambo ya kufundishia lakini kupitia jitihada za walimu ameweza kuelewa
vitu vingi katika fani hiyo.
Msopola
alisema mategemeo yake baada ya kumaliza mafunzo hayo ni kupata ajira kwani ana
matumaini kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya waendesha mitambo hiyo huku
akiongeza kuwa uzoefu unaonyesha kuwa vijana wengi wanapohitimu kozi hiyo
hupata ajira kwa urahisi katika makampuni mbalimbali.
Kozi ya muda
mrefu ya uendeshaji mitambo huchukua
miaka miwili na ile ya muda mfupi huchukua miezi miwili ambapo wanafunzi
wanaohitimu kozi hiyo hutegemea kuajirika
zaidi katika shughuli za utengenezaji barabara ,uchimbaji wa madini
pamoja na maeneo ya maliasili.
No comments:
Post a Comment