CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Monday 18 September 2017

TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUFUTIA USAJILI VYUO VILIVYOKIUKA TARATIBU ZA USAJILI ZA VETA




TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUFUTIA USAJILI VYUO VILIVYOKIUKA TARATIBU ZA USAJILI ZA VETA

   
 UTANGULIZI
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni chombo cha umma kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 1 ya mwaka 1994 [na kufanyiwa marekebisho mwaka 2006] kwa ajili ya kuratibu, kudhibiti ubora, kuendeleza, na kugharamia elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.

Usajili na Utoaji Ithibati kwa vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini ni miongoni mwa wajibu wa VETA katika kutekeleza jukumu la kuthibiti ubora wa mafunzo ya Ufundi stadi. Vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi nchini, vikiwemo vinavyomilikiwa na watu binafsi, taasisi binafsi, au umma vinapaswa kusajiliwa na kupata ithibati kutoka VETA kabla ya kuanza kutoa mafunzo.

VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUSAJILI
Vigezo vinavyotumika kusajili vyuo vinavyotoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi ni kama vifuatavyo:

  1. Mitaala: Chuo kinapaswa kutumia mitaala iliyoidhinishwa na Bodi inayosimamia Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi;

  1. Watumishi (Walimu na wasio walimu): Chuo kinapaswa kuwa na watumishi wa kutosha na wenye viwango vya elimu vinavyowiana na matakwa ya majukumu ya nafasi zao za kazi kama ilivyoanishwa katika miongozo ya kuanzisha vyuo;

  1. Zana na nyenzo za kufundishia:  Chuo kinapaswa kuwa na zana na nyenzo za kutosha kufundishia fani husika kama ilivyoainishwa katika miongozo;

  1. Miundombinu: Chuo hupaswa kuwa na miundombinu na mazingira yanayofaa na kukidhi vigezo vya utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kama ilivyoainishwa katika miongozo;

  1. Vyanzo vya fedha: Chuo hupaswa kuthibitisha kuwa kina vyanzo vya fedha vya kutosha na endelevu kwa ajili ya kutoa elimu na mafunzo yanayotarajiwa; na

  1. Huduma muhimu: Chuo hupaswa pia kuwa na huduma muhimu zikiwemo maji, umeme, mawasiliano, na usafiri.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                          
VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUTOA ITHIBATI
Vigezo vya kutoa ithibati kwa vyuo ni pamoja na:
  1. Mafunzo pendekezwa kuwa na mantiki na yenye kuhitajika kwenye soko la ajira;
  2.  Kuwa na miundo mbinu inayowezesha kutoa mafunzo kwa ufasaha na ufanisi;
  3.  Kuwa na zana na nyenzo bora za kufundishia; na
  4.  Kuwa na vifaa vya mawasiliano vinavyosaidia kutoa mafunzo.
  5. Kuwa na walimu wenye viwango vya elimu vinavyostahili kufundisha mafunzo husika;
  6. Kuwa na wanafunzi wenye uwezo wa kufuatilia mafunzo kulingana na mitaala husika;
  7. Kuwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa mafunzo;
  8. Kuwa na mifumo ya ndani ya kudhibiti ubora (internal quality assurance) wa mafunzo;
  9. Kuwa na utamaduni unaofaa wa uadilifu na uaminifu; na
  10. Uwezo wa kifedha na kukubalika kwa mafunzo kwenye soko la ajira pamoja na utawala bora wa chuo unaoshirikisha wadau.

MADARAJA YA USAJILI
Usajili hufanyika katika Madaraja manne yaani daraja A, B, C na D.  Vyeti vya usajili huonyesha daraja la usajili na fani zinazoruhusiwa kutolewa katika chuo kulingana na uwezo wake. Madaraja hayo na sifa zake ni kama ifuatavyo:

CATEGORY A
CATEGORY B
CATEGORY C
CATEGORY D

Chuo chenye uwezo wa   kutoa mafunzo kuanzia fani 8 kutoka sekta tofauti au zaidi na fani 4 kutoka sekta moja.  Angalau fani 4 kutoa  zaidi ya ngazi ya pili (level II)   
Chuo chenye uwezo wa kutoa kuanzia fani 5 toka kwenye sekta tofauti na fani 2 katika sekta moja. Angalau fani mbili kutolewa mpaka ngazi ya pili (level II)
Chuo chenye uwezo wa kutoa kuanzia fani   moja kuanzia kufikia ngazi ya pili (Level II). 
Chuo chenye uwezo wa kutoa mafunzo kuanzia moduli moja hadi kufikia ngazi ya kwanza ya mafunzo (Level I).  

Kwa hivyo, kwa mamlaka iliyonayo na kwa kuzingatia vigezo vya usajili na ithibati, VETA inautaaarifu umma kuwa vyuo vifuatavyo vimefutiwa usajili wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kutokana na kukiuka au kushindwa kutimiza vigezo na taratibu mbalimbali zinazotakiwa:


Na.

Jina la Chuo

Namba ya Usajili 

Sababu za Kufuta Usajili

Maagizo ya Hatua za Kuchukua
1.     
Starcom Hotel Academy - IRINGA
VET/IRA/PR/2012/C/030 
Kubadilisha eneo la kutolea mafunzo kutoka Kilolo kwenda eneo lingine la Iringa mjini ambalo halijaidhinishwa na VETA
Chuo kiombe upya usajili katika eneo jipya na kwa kuzingatia vigezo.
2.     
Southern College of Tanzania-IRINGA
VET/IRA/PR/2013/D/036


Kubadilisha eneo la kutolea mafunzo
Chuo kiombe upya usajili katika eneo jipya na kwa kuzingatia vigezo
3.     
Green House Technology VTC - DODOMA
VET/DOM/PR/2012/D/013

Mmiliki alifunga kituo bila ya kuiariBu ofisi ya VETA Kanda
Kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda
4.     
Amani VTC   DODOMA
VET/DOM/PR/2012/C/005

Kubadilisha chuo kuwa shule ya sekondari
Kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda
5.     
Mikukuyumbu VTC - MTWARA
VET/MTR/PR/2012/D/007

Kubadilisha chuo kuwa shule ya sekondari
Mmiliki anatakiwa kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda
6.     
Mnero VTC- LINDI
VET/LND/PR/2012/C/009


Upungufu wa zana na vifaa vya kufundishia pamoja na miundombinu kuwa chini ya kiwango

Kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda
7.     
Majority VTC -
MBEYA
VET/MBY/PR/2014/D/030

Kituo kilifungwa kutokana na mgogoro wa wamiliki
Kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda
8.     
Baraka VTC
DAR ES SALAAM

VET/DSM/PR/2012/D/003

Kubadilisha eneo la kutolea mafunzo kutoka Kinondoni Mkwajuni kwenda kwenye eneo lingine.
Chuo kiombe upya usajili katika eneo jipya na kuzingatia vigezo
9.     
Pure Academic of Aesthetics -
DAR ES SALAAM
VET/DSM/PR/2012/C/042


Kukosa wanafunzi kutokana na kutoza ada kubwa mno. Chuo kilikuwa kinatoza ada kubwa na kwa Dola za Kimarekani  
Kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda
10.  
Lamoon College of Business -
DAR ES SALAAM
VET/DSM/PR/2013/C/053
Kukosa Fedha Za Kuendesha Chuo.
Matumizi mabaya ya fedha yaliyosababisha uhaba mkubwa wa fedha za kuendeshea mafunzo  
Kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda
11.  
Mpera VTC -
SHINYANGA
VET/SHY/PR/2012/C/005


Kutozingatia vigezo vya usajili

Kurejesha cheti cha usajili kwenye ofisi ya VETA ya Kanda

WAMILIKI WOTE WA VYUO VYA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NCHINI WANAKUMBUSHWA KUZINGATIA VIGEZO, MASHARTI NA TARATIBU ZOTE ZA UTOAJI MAFUNZO NA UENDESHAJI WA VYUO KAMA ZILIVYOAINISHWA KATIKA MIONGOZI MBALIMBALI INAYOTOLEWA NA VETA. VETA HAITASITA KUCHUKUA HATUA STAHIKI KWA CHUO CHOCHOTE KITAKACHOENDELEA KUKIUKA MASHARTI NA TARATIBU ZA KUTOA MAFUNZO YA UFUNDI STADI.

LENGO LA HATUA HIZI NI KUHAKIKISHA KUWA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI YANATOLEWA KOTE NCHINI NI UBORA NA YANAZALISHA WAHITIMU WENYE STADI MAHIRI.

AIDHA WAZAZI NA WADAU WOTE WANAOMBWA KUWASILIANA NA OFISI ZETU ZA KANDA KATIKA MIKOA ILIYOORODHESHWA KWENYE JEDWARI ILI KUPATA TAARIFA ZA VYUO  VYA UFUNDI STADI KABLA YA KUPELEKA VIJANA WAO KUSOMA.

KANDA YA DSM    (D’SALAAM)
P.O.BOX 40274, DSM
Regional Director:
Habib Bukko
0784 584365
KANDA YA MASHARIKI (MOROGORO)
 P.O.BOX 1955, Morogoro
Regional Director:
Asanterabi M Kanza
0715 482952
kanzaamani@yahoo.com
vetaeasternzone@veta.go.tz
KANDA YA ZIWA – (MWANZA)
P.O.BOX 1983, Mwanza
Regional Director:
Hildegardis Bitegera
0754 384563
KANDA YA KATI (DODOMA)
P.O.BOX 2084, Dodoma
Regional Director:
Ramadhani Mataka
0784 365827
rmataka@veta.go.tz
KANDA YA KUSINI MAGHARIBI (MBEYA)
P.O.BOX 2498, Mbeya
Regional Director:
Justine Rutta
0784 263300
jrutta@veta.go.tz
KANDA YA MAGHARIBI (TABORA)
P.O.BOX 1218, Tabora
Regional Director:
Wilhard Soko
0754 429294
w_soko81@yahoo.com
wsoko@veta.go.tz
KANDA NYANDA ZA JUU  (IRINGA)
P.O.BOX 818, Iringa
Regional Director:
Suzana Magani
0784 358782
susanmagani@yahoo.com
KANDA YA KUSINI MAGHARIBI (MTWARA)                                 
P.O.BOX 700, Mtwara
Regional Director:
Kibehele Joseph
0713 232264
KANDA YA KASKAZINI   (MOSHI )
P.O.BOX 1738, Moshi
Regional Director:
Angelus Ngonyani
0773 150540

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
MKURUGENZI MKUU
VETA Makao Makuu
S.L.P. 2849, Dar es Salaam
Simu:  022 2863407/9
Baruapepe: info@veta.go.tz


Tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya VETA  www.veta.go.tz

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

MKURUGENZI MKUU
VETA Makao Makuu
S.L.P. 2849, Dar es Salaam
Simu:  022 2863407/9
Baruapepe: info@veta.go.tz

No comments:

Post a Comment