CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Tuesday, 14 August 2018

Jinsi ya Kujiunga na vyuo vinavyomilikiwa na VETA


VETA imeweka utaratibu maalum kwa ajili ya kujiunga ili kupata mafunzo katika vyuo inavyovimiliki. Utaratibu ni kama unavyoelezwa hapa chini:

VETA hutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika mifumo mbalimbali;

Kwa mafunzo ya muda mrefu, Vyuo vyote hutangaza nafasi za kujiunga mwezi wa Agosti kila mwaka. Matangazo hutolewa kupitia  vyombo mbalimbali vya habari nchini pamoja na kwenye tovuti ya www.veta.go.tz;

Mwombaji  lazima awe amemaliza elimu ya msingi, sekondari na kuendelea;

Mwombaji huchukua fomu katika chuo chochote cha VETA  kilichopo karibu naye . Fomu hizo zina taarifa ya vyuo vyote vinavyomilikiwa na VETA, ikiwa ni pamoja na fani zinazofundishwa na mahali chuo kilipo na kama ni kutwa au bweni;

Mwombaji anaruhusiwa kufanya mtihani wa kujiunga mkoa aliochukua fomu lakini anaweza kuchagua kusoma mkoa wowote anaochagua kulingana na mahitaji yake; 

Mwombaji anatakiwa kufanya mtihani wa kujiunga (Aptitude Tests) mwezi Oktoba na wale wanaofanikiwa kuchaguliwa hupewa taarifa mwezi Decemba ili kuanza masomo Januari mwaka unaofuata; 

Mwombaji anayefanikiwa hupewa barua ya kujiunga inayofafanua mahitaji yote muhimu. Mahitaji yanatofautiana toka chuo kimoja hadi kingine na kutegemeana na fani aliyoomba, na pia kama ni kutwa au bweni;

Kwa utaratibu huu Mwombaji anaanza kujiunga na daraja la 1(Level 1) ambalo ni daraja la chini. Waombaji wanaoendelea madaraja ya juu (Level II-III) vigezo ni ufaulu wa daraja husika unamwezesha kupanda daraja lingine.

 Aina ya fani na madaraja zitakazotolewa katika Vyuo vya VETA Mwaka 2019
 http://www.veta.go.tz/assets/uploads/c9c79-AINA-YA-FANI-NA-MADARAJA-ZITAKAZOTOLEWA-KATIKA-VYUO-VYA-VETA-MWAKA-2019..pdf 



No comments:

Post a Comment