Kamanda
wa kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Fortunatus
Musilimu amewataka madereva nchini kuchangamkia fursa za mafunzo ya udereva
bora katika vyuo mbalimbali ikiwemo vyuo
vya VETA.
Akizungumza
wakati wa mahafali ya mafunzo ya muda mfupi katika Chuo cha VETA Dar es Salaam
Kamanda Musilimu alisema zoezi la ukaguzi wa vyeti kwa madereva litafanyika
kama ilivyopangwa ambapo baada ya miezi mitano iliyotolewa na Jeshi la Polisi
kwa madereva kurudi shuleni na kupata vyeti kumalizika, hakutakuwa na mjadala
tena bali hatua stahiki zitachukuliwa.
“Nawakumbusha
madereva kuwa mwezi mmoja umeisha katika ile miezi mitano iliyotolewa….
Nawasihi tena kutumia vizuri muda uliobaki wakasome…”Alisema
Alisema
vyeti vyote vitatakiwa kuwa na sahihi ya Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa
ili kuhakikisha hakuna udanganyifu katika upatikanaji wa vyeti hivyo.
Kamanda
Musilimu aliwaasa vijana waliohitimu mafunzo katika chuo cha VETA kuhakikisha
wanatumia vyema ujuzi walioupata kuanzisha shughuli zao za kujiingizia kipato
kulingana na fani walizosoma.
Naye Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Stella Ndimubenya aliwataka vijana kutumia
vyema fursa zinazopatikana katika Halmashauri zao kuwa kuna fungu maalum kwa
ajili ya kuwawezesha vijana kufanya shughuli za ujasiriamali wakiwa kwenye
vikundi.
Awali, Mkuu
wa Chuo hicho Douglas Kipokola alisema chuo chake kwa kushirikiana na chuo cha
VETA Kihonda wamejipanga vyema kutoa mafunzo ya udereva bora kwa madereva wote
wataohitaji kupata mafunzo hayo.
Alisema
hivi karibuni chuo hicho kimeanza kutoa mafunzo kwa madereva wa magari
makubwa/malori yanayobeba mizigo na kwamba mtaala wake umeshapitishwa ambapo
mafunzo hayo yameanza kutolewa tarehe 3 Septemba mwaka huu huku kukiwa na
madereva 30 wanaopata mafunzo kwa wamu ya kwanza.
Kipokola
alisema katika mahafali hayo,jumla ya wanafunzi 1125 wamehitimu mafunzo ya muda
mfupi na katika fani mbalimbali ikiwepo Udereva, Uendeshaji wa hiteli, uhazili,
umeme, compyuta, mapishi, Nywele na urembo na ufundi wa magari.
No comments:
Post a Comment