Katika banda la VETA, wananchi wameweza kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na mafunzo ya Ufundi Stadi na kujionea ubunifu wa teknolojia na zana mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kilimo na kuongeza uzalishaji.Karibuni sana VETA.
Ujumbe “Kilimo,Mifugo,na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi"
Mkurugenzi
Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu akionyeshwa jinsi gani mashine ya kuchakata na
kukata majani kwa ajili ya malisho ya Mifugo
inavyofanya kazi. Mashine hiyo imebuniwa na mwalimu Fredrick Uliki wa chuo
cha VETA Kihonda na ina uwezo wa kuchakata tani saba kwa siku
Mkurugenzi Mkuu wa VETA
Dkt. Pancras Bujulu akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa fani ya Ushonaji
katika Chuo cha VETA Shinyanga Ester Singael(kwanza kushoto) alipotembelea banda
la VETA katika maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya
Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu 2019.Katika fani hii vijana
wanajifunza kushona nguo za watoto,za akina mama,wanaume,kudarizi,kutengeneza
taulo za kike ,Sabuni za aina mbalimbali na teknolojia ya vitambaa.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA
Dkt. Pancras Bujulu akipata maelezo kutoka kwa mwalimu Sussack Mbulu wa chuo
cha VETA Songea alipotembelea banda la VETA katika maonesho ya Nanenane
yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani
Simiyu. Mashine hiyo ya kubangua korosho ina uwezo wa kubangua debe tatu kwa
siku.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras
Bujulu (kushoto) akidadisi jambo juu ya mbegu za kupanda uyoga alipotembelea
banda la VETA katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja
vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu. Mkurugenzi Mkuu aliongozana na Meneja
uhusiano Sitta Peter (Katikati) na Mkurugenzi wa Kanda ya Magharibi Wilhard
Soko (Kulia)
No comments:
Post a Comment