Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Serikali alipotembelea mabanda Wabunifu wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Mfumo usio Rasmi kwenye finali za Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), leo tarehe 7 Mei 2021.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu Emmanuel Bukuku wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Dar es Salaam kuhusu Ubunifu wa Maabara ya Fizikia inayohamishika kwenye fainali Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ( MAKISATU). Mwalimu Bukuku anashiriki fainali za MAKISATU katika kundi la Vyuo vya Ufundi Stadi akiwa na Ubunifu wa Maabara hiyo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akijaribisha begi la shule lililotengenezwa kwa kutumia mabaki ya mifuko ya saruji. Mabegi hayo ambayo pia yana Mfumo wa kuchaji tochi na simu kwa kutumia nguvu ya jua (Solar) yamebuniwa na kikundi cha Soma Factory cha Mwanza. Soma Factory wanashiriki fainali za MAKISATU katika kundi la Mfumo usio Rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu akimpongeza Dkt. Abdallah Nyangalio, Mbunifu asiyeona aliyebuni Kifaa cha Kutungia Uzi na kufanikiwa kuingia fainali za MAKISATU kwa Ubunifu huo.
Ziara ya Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii kwenye Fainali za MAKISATU leo, tarehe 7 Mei 2021. Kulia ni Mwalimu Fredrick Uliki wa Chuo cha
Ufundi Stadi na Huduma Kihonda, akitoa maelezo kuhusu Ubunifu wa mashine ya
kusaga karanga.
Ernest Maranya kutoka
Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Dar es Salaam akiwaelezea Waheshimiwa Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Ubunifu wa
dawa ya fangasi. Wajumbe hao wametembelea Maonesho ya Ubunifu katika fainali za
MAKISATU, leo tarehe 7 Mei 2021.
Patrick Kitosi kutoka
Iringa, Mbunifu wa Mfumo usio Rasmi akitoa maelezo kwa Waheshimiwa Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu ubunifu wake
wa Mashine ya Kukusanya Sumu ya Nyuki. Wajumbe hao walitembelea Fainali za Mashindano
ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) leo, tarehe 7 Mei 2021
Waziri wa Elimu akiwa
katika Picha ya pamoja na wabunifu
No comments:
Post a Comment