CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Friday 19 April 2024

CPA Kasore: Kasimamieni utoaji mafunzo ya ufundi stadi kwa ubora kulingana na mahitaji ya soko la Ajira

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA. Anthony Kasore, amewaagiza wasimamizi wa mafunzo ya ufundi stadi kwenye vyuo vya VETA kuimarisha utoaji mafunzo ya ufundi stadi kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

CPA. Kasore ametoa maagizo hayo wakati wa kikao kilichowakutanisha wajumbe wa Menejimenti ya VETA Makao makuu, Wakurugenzi wa Kanda na wakuu wa vyuo vya VETA kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 19 Aprili, 2024.

Kasore amesema Serikali imeiamini VETA kutoa mafunzo ya ufundi stadi hapa nchini, hivyo ni wajibu wa watendaji wa VETA kutekeleza jukumu hilo kwa weledi.

 “nawahimiza kwa dhati kuwa mkatimize jukumu tulilonalo la kutoa mafunzo bora kulingana na mahitaji ya soko la ajira ili tuweze kuzalisha nguvukazi ya vijana bora katika fani,” amesema

CPA Kasore ameeleza kiu yake ya kuona watumishi wa VETA wanaimarisha ubora wa mafunzo na kasi ya utoaji mafunzo ili wananchi wote wapate mafunzo hayo kwa ubora  na hatimaye kuwa na nguvukazi mahiri kwa ajili ya kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi.






No comments:

Post a Comment