CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Saturday, 16 November 2024

MWENYEKITI VET BOARD AHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA VETA NA VIWANDA KATIKA KUWANOA VIJANA KIUJUZI

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufubdi Stadi (VET Board), Prof. Sifuni Mchome, ameeleza  umuhimu wa kuwa na ushirikiano kati ya VETA na viwanda katika utoaji elimu na mafunzo ya ufundi.

Akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainabu Telack, ofisini kwake, jana, tarehe 15 Novemba 2024, Pro. Mchome akiwa na wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya VETA amesema, katika kuhakikisha VETA inatoa wahitimu bora, kuna haja ya kuwa na ushirikiano na viwanda ili wanafunzi waweze  kupata mafunzo kwa vitendo sehemu za kazi na kuongeza umahiri katika fani zao.

Aidha, Prof. Mchome, ametoa wito Kwa wakazi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa za mafunzo ya Ufundi Stadi yanayotolewa na vyuo vya VETA, hasa ikizingatiwa kuwa gharama zake ni ndogo licha ya umuhimu wake katika kuwezesha vijana kuajirika kwa urahisi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack amepongeza mpango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali wananchi katika kuwajengea vyuo vya Ufundi Stadi katika kila wilaya.

Ameitaka VETA kufanya kazi ya ziada kujitangaza ili vijana wengi waweze kujiunga na kupata ujuzi wa Ufundi Stadi.

Amesema kuna haja ya kutoa elimu Kwa wananchi kuhusiana na suala la gharama za mafunzo ili kuondoa dhana ya kuwa gharama yake ni kubwa.

Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board), imefanya ziara na  kukagua shughuli za utoaji mafunzo katika chuo cha VETA Ruangwa, mkoa wa Lindi  na mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, tarehe 15 Novemba 2024.


 

No comments:

Post a Comment