Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Kampuni ya Fundi Smart ya jijini Mbeya
zimetiliana saini makubaliano ya kushirikiana kutoa mafunzo ya Ufundi na
kuwezesha urasimiahaji wa mafundi waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi wa
mafunzo.
Makubaliano hayo
yamesainiwa jana, tarehe 6 Decemba 2024, katika ukumbi wa VETA Makao Makuu,
jijini Dodoma kati ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA.Anthony Kasore na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Fundi Smart, Fredy Herbert Pole.
Wote Kwa pamoja
wamekubaliana kuanzisha na kutoa mafunzo Kwa mafundi wasio rasmi (Wanagenzi) na
hatimaye kuwarasimisha na kuwatambua kwa viwango vinavyohitajika kwenye stadi
husika.


.jpeg)
No comments:
Post a Comment