Waziri Mkuu mstaafu, Mhe.
Mizengo Pinda ameelezea kufurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika utoaji wa mafunzo ya ufundi
stadi yanayowawezesha Watanzania wengi kupata ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa.
Pinda ameyasema hayo jana 20
Machi, 2025 katika maadhimisho ya miaka 30 ya VETA ambapo pia alitembelea
mabanda mbalimbali kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Amebainisha kwamba ufundi stadi
ni sehemu ya maisha ya mwanadamu ambapo maendeleo ya Taifa yanategemea ujuzi
ambao hakuna mtu anayeweza kukwepa, na amepongeza VETA kwa kazi kubwa
waliyoifanya tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo.
“Tumeona mambo mengi mazuri, yanaonyesha dhahiri kwamba tulikokuwa siko tulipo, tumepiga hatua kubwa katika ufundi stadi pamoja na ubunifu mambo ambayo katika maisha ya mwanadamu hawezi kuyakwepa, ni sehemu ya maisha ya mtu, ni sehemu ya maendeleo ya taifa.”
Aidha,ameongeza kwamba,“VETA
mnastahili kupewa pongezi kwa kazi kubwa ambayo mmeifanya mpaka sasa, ndani ya
mafunzo yanayotolewa utakuta kilimo kipo, ufugaji upo, uvuvi upo. Ukitazama
kwenye huduma za jamii afya, elimu yenyewe na vitu vingine mafundi stadi
wametoka kwenye vyuo vyetu,”




No comments:
Post a Comment