CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Wednesday 24 May 2017

VETA KIPAWA YATOA MAFUNZO YA UMEME KWA WAFANYAKAZI 78 WA KAMPUNI YA PIVOTECH

Jumla ya wafanyakazi 78 wa kampuni ya PIVOTECH wamehitimu mafunzo ya muda mfupi ya fani ya umeme katika chuo cha VETA Kipawa.

Wafanyakazi hao walipatiwa vyeti vyao vya kuhitimu katika hafla iliyofanyika jana tarehe 17 Mei, 2017 chuoni hapo.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Harold Mganga, uamuzi wa kampuni hiyo wa kuwaleta wafanyakazi wake kupata mafunzo hayo ulitokana na aina ya shughuli kampuni hiyo inazozifanya kuhitaji kuboresha ujuzi wa umeme na kukidhi vigezo na matakwa ya mamlaka za uthibiti kama EWURA.

Alisema,ufungaji wa mifumo ya umeme ni shughuli mojawapo inayohitaji mtu anayefanya kazi hiyo kuwa na Leseni,ambayo kutolewa kwake kunahitaji mtu awe amefuzu mafunzo ya ufundi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa PIVOTECH Mark Anthony Cresswell alishukuru uongozi wa VETA Kipawa kusimamia vyema mafunzo hayo huku akiamini kuwa wafanyakazi hao wataleta mchango mkubwa katika kuboresha shughuli wanazozifanya na kuongeza tija katika kampuni.
Kampuni ya PIVOTECH inashughulika na kazi mbalimbali za kiufundi ikiwemo ufungaji wa minara, ujenzi wa barabara na ufungaji wa viyoyozi.


No comments:

Post a Comment