CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Thursday 4 May 2017

Vijana Wanagenzi Kutoka VETA Waenda Ujerumani




Wahitimu watatu waliofanya vizuri zaidi katika Mpango wa Mafunzo ya Uwanagenzi Pacha (Dual Apprenticeship training programme) unaoendeshwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA kwa ushirikiano na Ujerumani wamepata ufadhili wa ziara ya mafunzo nchini Ujerumani, kama sehemu ya tuzo kwa kufanya vyema zaidi katika mafunzo yao.


Wahitimu hao wa uwanagenzi waliondoka jana 2 Mei, 2017 na watakuwa nchini Ujerumani kwa muda wa mwezi mmoja.

Wahitimu hao ni Irene Ndauka (Hoteli na Utalii) kutoka Moshi, Simba Mandela (Ufundi Magari) Dar es Salaam na Mariam Zayumba (Ufundi Umeme) Dar es Salaam.

Wahitimu hao waliagwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dr Bwire Ndazi, Mkurugenzi wa Mafunzo LeahDotto Lukindo pamoja na wasimamizi wakuu wa mradi huo baada ya kukabidhiwa vyeti vyao vya kuhitimu.

Mradi huu unatekelezwa na VETA kwa kushirikiana na Hamburg Chamber of Skilled Craft ya nchini Ujerumani







No comments:

Post a Comment