CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Thursday 15 June 2017

Namna Mafunzo kwa njia ya Simu-VSOMO yanavyotolewa













Mafunzo kwa njia ya simu yamebuniwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa lengo la kupanua wigo wa mafunzo ya ufundi stadi na kurahisishia watu wengi kujifunza na kupata ujuzi. 

Mafunzo haya kwa sasa yanahusisha kozi za muda mfupi.

Utaratibu wa mafunzo umegawanyika katika sehemu mbili:
1. Mafunzo ya nadharia ambayo hutolewa kupitia simu za mkononi-Simu za kupangusa-smartphone.
2. Mafunzo kwa vitendo ambayo hutolewa katika vyuo vya VETA.

Mlolongo wa mafunzo ni kuwa, mtu anayetaka kujiunga huanza kwa kupakua application ya VSOMO kwenye google play store( http://airtelfursa.com/vsomo/.) Kisha hujisajili kwa kutumia namba ya Airtel na kuchagua aina ufundi/ujuzi anaotaka kujifunza. 

Katika simu yake atapata notice na kujisomea. Baada ya kujisajili anaweza kusoma notice hata kama hayuko kwenye mtandao wa internet. Internet inahitajika wakati wa kujisajili tu.

Mwisho wa kila hatua-module, kuna majaribio na mitihani ambayo unapaswa kuifanya na kufaulu kabla ya kuhamia kwenye hatua nyingine. Mitihani husahihishwa kwa mfumo wa kompyuta. Ikiwa hujafaulu, mfumo utakuzuia kuendelea hatua inayofuata hadi ufaulu.

Baada ya kukamilisha hatua zote na kufaulu mitihani yote ya nadharia kwenye simu, mwanafunzi hutakiwa kuchagua chuo cha VETA kilicho karibu naye au kile anachopenda kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo. Mfumo humtaarifu na kumpa orodha ya vyuo vilivyopo ili ajaze na kufanya booking ya mafunzo ya vitendo.

Mfumo wa kompyuta hutoa pia taarifa kwenye chuo juu ya wanafunzi wanaotarajiwa kufika kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.
Mwanafunzi afikapo chuoni hufanyishwa kwanza mtihani wa majaribio ili kuhakikisha kama kweli ni yeye aliyekuwa akisoma kwenye simu. Baada ya kufaulu mtihani huo ndipo huanza rasmi mafunzo kwa vitendo.

Mwanafunzi hukaa katika mafunzo ya vitendo kwa walau wiki mbili na kila siku hutakiwa kutumia walau masaa 6 akijifunza kwa vitendo. Kwa hivyo baada ya wiki mbili anakuwa amekamilisha masaa ya mafunzo ya vitendo yapatayo 60.

Hatimaye hupewa mtihani wa mwisho na akifaulu hutunukiwa cheti.



1 comment:

  1. Dah mfumo nimeupenda nahitaji kujifunza ufundi simu je mafunzo haya yapo

    ReplyDelete