Mamlaka ya elimu
na Mafunzo ya ufundi Stadi
(VETA) kwa kushirikiana Kampuni ya simu ya mkononi Airtel kupitia
application ya VSOMO wamewatunuku vyeti vijana zaidi ya saba walio hitimu
mafunzo hayo kwa njia ya simu.
Akikabidhi vyeti
hivyo ,Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam, ndugu Habibu Bukko aliishukuru
kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa
kushirikiana nayo kupitia application ya VSOMO kwani application hiyo imeweza
kusaidia wanafunzi kwa kiasi kikubwa hasa wale walio mbali na vyuo vya Ufundi
stadi.
Alisema
jitiahada za kutoa masomo ya ufundi stadi kupitia application ya VSOMO
zinaendana na mikakati iliyojiwekea VETA na serikali kutanua wigo wa kutoa
mafunzo ya ufundi stadi.
Alisema Application
hii inalenga kufikia vijana walio mbali yaani vijijini ambapo kwao ni ngumu
kufikia huduma ya vyuo vya ufundi stadi vya karibu lakini pia sehemu ambapo
kuna miundombinu hafifu.
Pia aliwapongeza
vijana hao kwa kutumia vyema simu zao za mkononi kwa ajili ya masomo.
Akiongea na
waandishi Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtell Tanzania Beatrice Singano alisema
Airtell wanayo furaha kubwa sana katika kusaidia vijana kupata mafunzo ya
Ufundi stadi,
Alisema kwa
kupitia programu hii wana uhakika nchi itapata mafundi bora na nguvu kazi ya
kutosha kwani wamejifunza kuwa vijana wanaopitia mafunzo haya ni makini na
wenye uwezo mkubwa.
Aliendelea
kuwahamasisha vijana kudownload application ya VSOMO Kwenye simu zao ili kuweza
kupata fursa ya kuweza kupata mafunzo kwa njia rahisi sana.
Naye mwakilishi wa mkuu wa chuo cha VETA Kipawa,Harold Mganga, alisema Mpango huu umevutia vijana zaidi ya 30,000 ambao wameweza kupakua aplication ya VSOMO na kati yao, 9,000 wamejiandikisha kwa masomo
Alisema programu ya VSOMO ina lengo la kupanua vikwazo
vya VETA kutoa masomo ya ufundi kwa jamii kote nchini.
"Hadi sasa tuna wanafunzi 54 ambao wamekamilisha
kozi zao za ufundi na wametunukiwa vyeti," alisema na kuongeza,“hivi
karibuni tutakuwa na kundi lingine la wanafunzi wanaomaliza masomona tayari
tuna wanafunzi 25 wanasubiri mafunzo ya vitendo yaliyotarajiwa kuanza hivi
karibuni katika vyuo vyetu vya VETA .”
Aliwahimiza vijana kujiandikisha kwa ajili ya mafunzo ya
ufundi kupitia simu zao za mkononi na VETA watakuwa katika huduma yao ili
kuhakikisha kuwa wanafuatilia mafunzo kwa viwango vya kazi.
No comments:
Post a Comment