CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Thursday 5 April 2018

Matukio katika picha ni ziara ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipotembelea katika chuo cha VETA Mwanza tarehe 26 Machi na VETA Shinyanga tarehe 28 Machi 2018 . Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mh. Naghenjwa Kaboyoka.




Mkuu wa Chuo cha VETA Mwanza, Charles Kengese (anayenyoosha mkono) akionesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya karakana ya mafunzo ya ufundi wa umeme wa viwandani wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika chuo cha VETA Mwanza, 26 Machi, 2018. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa PAC Mh. Naghenjwa Kaboyoka na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Peter Maduki. Wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo na maafisa mbalimbali wa serikali na Menejimenti ya VETA.





Mkufunzi wa Chuo cha VETA Shinyanga, Florence Kihundo (kushoto) akiwaelezea  wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ubunifu wa utengenezaji wa samani na vifaa mbalimbali kwa kutumia maranda ya mbao, ambao unasaidia utunzaji wa mazingira kwa kupunguza utupaji hovyo wa maranda, wakati Kamati hiyo ilipotembelea katika chuo cha VETA Shinyanga, tarehe 28 Machi, 2018. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa PAC, Mh. Aeshi Hilaly akiangalia kwa makini moja ya vifaa hivyo.



Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt. Bwire Ndazi (aliyesimama) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) juu ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya Mamlaka wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika chuo cha VETA Mwanza, 26 Machi, 2018. Kulia na kushoto kwake ni maafisa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.





Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Peter Maduki (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Mafunzo ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa yanayoendeshwa katika Chuo cha VETA Shinyanga wakati Kamati hiyo ilipotembelea karakana ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa katika chuo hicho, tarehe 28 Machi, 2018. Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa PAC Mh. Aeshi Hilaly.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakisikiliza maelezo juu ya stadi za ukataji na ung’arisha madini na vito, kutoka kwa mwanafunzi wa kozi hiyo katika chuo cha VETA Shinyanga, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye chuo hicho tarehe 28 Machi, 2018.



Mkuu wa chuo cha VETA Shinyanga, Afridon Mkhomoi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Mafunzo ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa yanayoendeshwa katika Chuo cha VETA Shinyanga wakati Kamati hiyo ilipotembelea karakana ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa katika chuo hicho, tarehe 28 Machi, 2018. Kulia mwisho ni Makamu Mwenyekiti wa PAC Mh. Aeshi Hilaly na kushoto mwisho ni Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Peter Maduki.




Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mh. Naghenjwa Kaboyoka (wa pili kutoka kushoto-mbele) akitoa maneno ya pongezi kwa VETA baada ya kutembelea na kujionea ujenzi wa karakana ya Mafunzo ya Ufundi wa Umeme wa Viwandani katika chuo cha VETA Mwanza, tarehe 26 Machi, 2018. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Peter Maduki na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha VETA Mwanza, Charles Kengese.

No comments:

Post a Comment