CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Friday 4 May 2018

Wasichana wahamasishwa kujiunga na kozi ya Uendeshaji Mitambo


Wasichana nchini wameshauriwa kujiunga na kozi ya uendeshaji mitambo inayotolewa katika chuo cha VETA Shinyanga ili kujipatia ajira kwa urahisi na kujikwamua kiuchumi kutokana na fani hiyo kuwa na  fursa nyingi katika soko la ajira.

Akizungumza chuoni hapo, Mkufunzi wa Uendeshaji mitambo mikubwa Aclay Fraten alisema mwitikio wa wasichana kusoma kozi hiyo bado ni mdogo sana ukiliganisha na wavulana.

Kwa mujibu wa Mwalimu Fraten kati ya wanafunzi 149 wanaosoma fani hiyo wasichana ni 11 tu na kwamba changamoto inatokana na dhana iliyojengeka  kuwa  kazi za mitambo ni za wanaume pekee
“Imefikia wakati wa kubadili mtizamo na kuona fani hiyo hata wasichana wanaweza na sio kuwaachia wavulana tu.

Mmoja wa mwanafunzi wa kozi ya Uendeshaji wa Mitambo kutoka mkoani Morogoro, Happiness Msopola alisema alitamani kujua uendeshaji wa mitambo siku nyingi na kwamba ni kozi anayoipenda kutoka moyoni, lakini hakuwa na taarifa kozi hiyo inapatikana wapi hadi  alipopata taarifa kuwa inapatikana Chuo cha VETA Shinyanga. 

Alisema kuwa kozi hiyo ni rahisi tofauti na baadhi ya wasichana wengi  wanavyodhani kuwa kozi hizo ni kwa wanaume pekee“Tena naona hii kozi inawafaa zaidi wanawake, maana hata uendeshaji wake si mgumu, kwa hiyo nawashauri wanawake wenzangu wajifunze hii kozi ili tuweze kujikwamua na maisha. ….. Ninawaomba waajiri watuamini, wasione tu kwamba pengine wanatuajiri kwa kutusaidia kwa sababu ni wanawake. Watuajiri wakijua kuwa wanaajiri watu mahiri na wanaojiweza.,” alisema.

Alisema  wakati anaanza  kusoma kozi hiyo hakuwa na uelewa wa kifaa chochote katika mitambo ya kufundishia lakini kupitia jitihada za walimu ameweza kuelewa vitu vingi katika fani hiyo.

Msopola alisema mategemeo yake baada ya kumaliza mafunzo hayo ni kupata ajira kwani ana matumaini kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya waendesha mitambo hiyo huku akiongeza kuwa uzoefu unaonyesha kuwa vijana wengi wanapohitimu kozi hiyo hupata ajira kwa urahisi katika makampuni mbalimbali.

Kozi ya muda mrefu ya uendeshaji mitambo  huchukua miaka miwili na ile ya muda mfupi huchukua miezi miwili ambapo wanafunzi wanaohitimu kozi hiyo hutegemea kuajirika  zaidi katika shughuli za  utengenezaji barabara ,uchimbaji wa madini pamoja na maeneo ya maliasili. 


No comments:

Post a Comment