CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Sunday 4 August 2019

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda la VETA kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Katika banda la VETA, wananchi wataweza kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na mafunzo ya Ufundi Stadi na kujionea ubunifu wa teknolojia na zana mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kilimo na kuongeza uzalishaji.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu “Kilimo,Mifugo,na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi" yalizinduliwa tarehe 1 Agosti 2019 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 8 Agosti 2019.

No comments:

Post a Comment