Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshiriki Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenye Viwanja vya Jamhuri, Jijini Dodoma, tarehe 27 Mei hadi tarehe 2 Juni 2021. Katika Maonesho hayo, VETA imewakilishwa na vyuo vyake vinavyotoa kozi zenye ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Vyuo vilivyoshiriki ni Chuo cha TEHAMA cha VETA Kipawa, Chuo cha VETA cha Hoteli na Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha), Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC) na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma Dar es Salaam.
Mhandisi Frank
Urio, Mkufunzi wa Kozi ya Umeme, katika Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi
Morogoro (MVTTC), upande wa kulia, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la VETA, juu ya
matumizi ya mitambo ya kufundishia umeme (simulators) inayotumiwa na chuo hicho
kuimarisha utoaji wa wa mafunzo kwa vitendo.
Mhandisi Frank
Urio, Mkufunzi wa kozi ya Umeme, katika Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi
Morogoro (MVTTC), upande wa kushoto, akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia, Prof. James Mdoe, juu ya matumizi ya mitambo ya kufundishia
umeme (simulators) inayotumiwa na chuo hicho kuimarisha utoaji wa wa mafunzo
kwa vitendo.
Naibu Katibu
Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe (Kushoto, mbele)
akisikiliza maelezo kutoka kwa Marynurce Kazosi, Mkufunzi wa kozi ya Afya na
Lishe ya Chakula katika Chuo cha Hoteli na Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha), kuhusu
mafunzo yanatotolewa na chuo hicho kwenye kozi ya Uandaaji wa Chakula. Prof.
Mdoe alitembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya Pili Vyuo vya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, tarehe 29 Mei 2021.
Baadhi ya watu
waliotembele banda la VETA kwenye Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi kwenye Viwanja vya Jamhuri, Jijini Dodoma wakifurahia vinywaji
vilivyoandaliwa na Chuo cha VETA cha Hoteli na Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha)
ikiwa ni sehemu ya kuonesha umahiri wa walimu na wanafunzi katika eneo la
huduma za hoteli na utalii.
Kulthumu Sato
(kushoto), Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Dar es Salaa, Fani ya
Nguo na Ubunifu wa Mitindo ya Mavazi akieleza kuhusu mafunzo ya Fani ya Nguo na
Ubunifu wa Mitindo ya Mavazi kwa watu waliotembelea banda la VETA kwenye
Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Uwanja wa Jamhuri,
Jijini Dodoma.
Farida Kondo Mkilalu,
Mwanafunzi wa Chuo cha TEHAMA Cha VETA Kipawa akiwaelezea wananchi
waliotembelea Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu
mfumo uliobuniwa na chuo chake kurahisisha uchakataji wa mauzo na faida katika
biashara.
Meneja
Uhusiano wa VETA, Sitta Peter (katikati) akifanya mahojiano na wandishi wa habari
kuhusu ushiriki wa VETA kwenye Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi.
Marynurce
Kazosi, Mkufunzi wa kozi ya Afya na Lishe ya Chakula katika Chuo cha Hoteli na
Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha), akifafanua kuhusu mafunzo ya chuo hicho kwa watu
waliotembelea Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Uwanja
wa Jamhuri, Jijini Dodoma.
Bellington
Lyimo, Mbunifu wa Vifaa vya Maabara (katikati) akiwaonesha wanafunzi moja ya
kifaa alichobuni kinavyofanya kazi katika kujifunza kwa vitendo.
No comments:
Post a Comment