CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Friday, 6 August 2021

VETA yakabidhi vifaa vya milioni 62 kwa vyuo binafsi


 Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia VETA Kanda ya Kati imetoa vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya Shilingi Milioni 62.8 kwa vyuo vya Ufundi Stadi vinavyomilikiwa na watu binafsi, Mashirika ya Dini na Mashirika ya Kijamaa.

Akikabidhi vifaa hivyo katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 3 Agosti, 2021, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati Bw. John Mwanja amesema uwezeshaji huo unalenga kuboresha utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi katika kanda hiyo, kuongeza udahili na kuwezesha vyuo kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Amesema VETA inatambua mchango mkubwa unaotolewa na vyuo binafsi katika kuwapatia vijana ujuzi na hivyo imeona ni vyema kuviongezea nguvu vyuo hivyo ili viweze  kujiimarisha katika kutoa mafunzo.


"Tunaamini kupitia vifaa hivi tulivyovitoa leo utoaji mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi utaenda kuboreka na hatimaye kuandaa vijana wetu ili waweze kuhitimu wakiwa na stadi mahiri zitakazowawezesha kujipatia ajira na kukuza uchumi," alisema

Naye Mratibu wa Vyuo vya Ufundi Stadi Kanda ya Kati, Bi Joyce Mwang’onda, alisema vifaa hivyo vimekuwa vikitolewa kwa awamu na kutaja vyuo vilivyonufaika kuwa ni Don Bosco VTC,  St.Gabriel VTC, St.Ursula Ludochowaski, Sema VTC, na Veyula VTC.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Don Bosco Bw. Auson Ntoba alisema vifaa hivyo vitainua hamasa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo zaidi .

Naye Mkuu wa chuo cha St. Ursula VTC Sista Josephina  Mbori aliishukuru VETA kwa msaada huo wa vifaa na kuahidi kuvitumia vyema kutoa ujuzi kwa wanafunzi chuoni hapo.



No comments:

Post a Comment