Mkurugenzi Mkuu wa
VETA, CPA Anthony Kasore, ameiagiza
Kamati ya Ushauri Sekta ya Ukarimu VETA Kanda ya kati kusimamia malengo
waliyojiwekea ili kutatua changamoto mbalimbali zinahusiana na sekta ya ukarimu
na utalii.
CPA Kasore ametoa maagizo hayo alipokuwa akizundua kamati hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya VETA Dodoma tarehe 30 Desemba, 2024.
Amesema kuwa kamati hiyo inapaswa kutambua watu wanaofanya kazi katika sekta hiyo ambao hawajapata mafunzo ili kuweza kurasimisha ujuzi wao waliopata bila kupitia mafunzo rasmi.
CPA Kasore amesema ni
vyema hoteli ziwe na Darasa la kufundishia kwa vitendo kama ilivyo hoteli za
VETA ili kurahisa wanafunzi wanao kwenda huko kujifunza kwa urahisi.
“Hoteli yetu ya hapa Dodoma ina darasa kwaajili ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo ili kuongeza wigo wanafunzi kujifunza kwa vitendo ningependa kuona hoteli nyingine nchini nazo zinakuwa na sehemu ya darasa la kujifunzia” amesema CPA Kasore
Aidha, CPA kasore ameitaka kamati hiyo kushirikiana na walimu kutoka VETA kuandaa makongamano na kuwakutanisha wanafunzi ili kubadilishana uzoefu katika eneo hilo la Ukarimu na utalii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati, Ramadhani Mataka, amesema VETA kanda ya kati itaendelea kujikita katika kutoa mafunzo kwa vitendo na kuitaka kamati hiyo kufanikisha wanafunzi wa Ukarimu na Utalii wanapata mafunzo kwa vitendo pindi unapofika wakati wa kujifunza kwa vitendo.
Naye, Mwenyekiti wa kamati hiyo Wellington Maleya amasema kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati hiyo watahakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo waliojiweke na matarajio ya VETA kwa mujibu wa miongozo iliyopo..
Kamati hiyo ya ushauri Sekta ya Ukarimu na Utalii VETA Kanda ya kati imetokana na kongamano la wadau wa Sekta ya Ukarimu na Utalii Mkoa wa Dodoma, Kongamano hilo liliandaliwa na Ofisi ya VETA Kanda ya Kati kwa kushirikiana na chuo cha VETA Dodoma, lilikuwa na lengo la kuwakutanisha wadau wa sekta ya ukarimu na utalii na chuo cha VETA Dodoma ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta hiyo..




No comments:
Post a Comment