CPA Kasore amesema hayo leo tarehe 31 Desemba 2024 alipokuwa akitoa salamu za kufunga mwaka 2024 na kupokea mwaka 2025 kwa watumishi wa VETA Makao Makuu Jijini Dodoma, wakiwawakilisha watumishi VETA kote nchini.
“Katika kutekeleza majukumu
yetu sisi VETA tunatakiwa kuhakikisha watanzania wanapata ujuzi ili waweze
kujiajiri au kuajiriwa ili kuwawezeshakujipatia kipato chao cha kila siku
kutokana na ujuzi walioupata VETA na hilo litawezekana kama tutakuwa na nia moja
katika kutimiza malengo yetu” amesema CPA Kasore.
Aidha Mkurugenzi Mkuu amesema matarajio ya Watanzania wengi ni kuona mafunzo ya Ufundi Stadi yanayotolewa VETA yanawasaidia kuwatoa katika maisha ya kawaida.
Sambamba na hilo CPA
Kasore amewataka watumishi wa VETA kote
Nchini kuendelae kufanya kazi kwa nguvu, jitihada na ari.
Amesisitiza kuwa kila idara na mtumishi wa VETA ana malengo yake, na hivyo ni muhimu kuhakikisha malengo haya yanatimizwa.
Ameeleza mafanikio ya mwaka 2024, akisema kuwa idadi ya vyuo vya VETA imeongezeka na ujenzi wa vyuo 65 unaendelea, huku lengo la kufikia vyuo 145 ifikapo mwaka 2025 likiendelea kutekelezwa.
CPA Kasore
amesisitiza pia umuhimu wa kutoa mafunzo ya amali kwa wanafunzi wa sekondari
ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi.
CPA Kasore
amehitimisha salamu zake za mwaka mpya kwa kutoa shukurani kwa Mheshimiwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na
kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA mwezi Aprili 2024.
Alisema kuwa
ushirikiano na umoja kati ya VETA na Bodi yake, inayoongozwa na Profesa Sifuni
Machome, umeleta mafanikio makubwa katika kipindi cha mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment