CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Tuesday 24 April 2018

Swissport yaajiri vijana 178 kutoka VETA


Kampuni ya Swissport inayojishughulisha na utoaji wa huduma katika viwanja vya ndege nchini imeajiri vijana 178 kutoka vyuo mbalimbali vya VETA katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kubaini kuwa vijana hao wana ujuzi na uadilifu katika kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport nchini Mriso Bakari Yassin aliyabainisha hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mjini ofisi za Swissport katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Yasini alisema kuwa kati ya vijana hao 150 wametoka chuo cha VETA Dar es Salaam na 28 wametoka chuo cha VETA Moshi.

“Kwa sasa Swissport tunaamini zao la VETA ni zao bora kwa shughuli zetu na tutaendelea kuwatumia wahitimu wa VETA kwa kadri tutakavyokuwa tunahitaji wafanyakazi,” alisema.

Aliongeza kuwa baada ya kujenga imani kubwa kwa VETA na vijana wake, kampuni yake inafikiria kuingia makubaliano na VETA ili ikasimishe kwake kazi ya usafi katika viwanja vya ndege inavyovihudumia, kwa kuwa inafundisha pia kozi ya usafi.  

Aliwashauri waajiri wengine kuwaamini na kuwatumia vijana kutoka VETA kwani ni vijana mahiri na waadilifu katika kazi.





No comments:

Post a Comment