Wananchi mbalimbali
jijini Mbeya wamejitokeza kutembelea banda la VETA na kupata elimu juu ya fursa
za mafunzo zinazopatikana katika vyuo vya VETA nchini wakati wa maonesho ya
Mifuko ya Uwezeshaji, Taasisi na Vikundi vya Kifedha.
Maonesho hayo
yanafanyika jijini Mbeya katika viwanja vya shule ya msingi Ruanda Nzovwe
kuanzia Oktoba 19 hadi 23, 2018 yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya
fursa zinazopatikana katika taasisi na mifuko mbalimbali ya uwezeshaji za serikali
na binafsi.
Akizungumza katika
maonesho hayo Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mbeya Mhandisi Hassan Kalima amesema
ushiriki wa VETA kwenye maonesho hayo umelenga kuwaelimisha wananchi na
wajasiriamali juu ya fursa za mafunzo zinazopatikana katika vyuo vya ufundi
stadi nchini na namna wanaweza kuzifikia fursa hizo.
Mhandisi Kalima
aliwataka wananchi wa jiji la Mbeya kuchangamkia fursa za mafunzo katika chuo
cha VETA Mbeya ili waweze kujipatia ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au
kuajiriwa na kuchangia katika nchi ya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia
viwanda.
Mmoja wa wananchi
aliyetembelea banda la VETA Benjamini Machaule amesema elimu inayotolewa na
VETA katika maonesho hayo imemjengea uelewa juu ya elimu ya ufundi stadi na
fursa zinazopatikana baada ya kujipatia elimu hiyo hasa uwezo wa kujiajiri
mwenewe bila kutegemea kuajiriwa.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea banda la VETA wakipewa elimu kutoka kwa mmoja wa
wanafunzi wa chuo cha VETA Mbeya katika maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji,
taasisi na vikundi vya kifedha yanayo fanyika katika viwanja vya Shule ya
Msingi Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Mkuu wa Chuo Cha VETA Mbeya (Katikati) Mhandisi
Hassan Kalima akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la
VETA kwenye maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji,Taasisi na vikundi vya kifedha
yanayofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya
Wananchi
waliotembelea banda la VETA wakipewa elimu namna ya mfumo wa umeme kwenye
injini ya gari kwenye maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji,Taasisi na vikundi vya
kifedha yanayo fanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la VETA
wakipewa elimu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa chuo cha VETA Mbeya katika
maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji, taasisi na vikundi vya kifedha yanayo fanyika
katika viwanja vya Shule ya Msingi Ruanda Nzovwe jijini Mbeya
No comments:
Post a Comment