WAZIRI wa Viwanda
Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema ni vyema Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuanza kuwekeza katika kubuni teknolojia za
kisasa na kuzalisha mashine za kurahisisha shughuli za viwanda nchini.
Kakunda aliyasema
hayo alipotembelea banda VETA katika Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda
Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere-Sabasaba jijini Dar
es Salaam.
Amesema kutokana na
mkakati wa serikali kwenda katika uchumi wa kati kupitia viwanda, VETA inawajibu wa kuzalisha nguvu kazi yenye uwezo
wa kubuni teknolojia ambazo zitarahisisha kufanya uchakataji wa malighafi zinazolishwa
nchini.
Kakunda amesema kuwa mali ghafi zikichakatwa
nchini zitasaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa malighafi hizo na hatimaye
kuwasiadia wakulima kunufaika na kilimo wanachokifanya.
“VETA mna nafasi
kubwa nchini katika maendeleo ya viwanda na serikali inawategemea katika
uzalishaji wa teknolojia na nguvu kazi ili kusaidia kusukuma maendeleo hayo,”
alisema.
Maonesho ya tatu ya
bidhaa za viwanda yanafanyika katika viwanja vya Sabasaba kuanzia tarehe 5 hadi
9 Desemba 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph
Kakunda akipata maelezo kutoka kwa Afisa Habari wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) David Edward
wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za
Viwanda Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment