Mamlaka
ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi VETA, imeingia makubaliano na kampuni ya
SIKA Tanzania Construction Chemicals Ltd hapo tarehe 1/03/2019 ambayo yana
lengo la kuwaongezea uwezo walimu na wanafunzi katika kuboresha mitaala ya VETA
kwa fani za Ujenzi, mafunzo katika matumizi ya teknolojia mpya, na uboreshwaji
wa karakana za kufundishia katika chuo cha VETA Dar es salaam.
Akizungumza
wakati wa kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa VETA DKT.PACRAS BUJULU
alisema madhumuni ya kuingia makubaliano hayo na kampuni ya SIKA ni kuweza
kuwasaidia vijana ili kuweza kuwaongezea sifa za kuajirika kimataifa na kuweza
kutambua teknolojia za kisasa zinazo tumika katika viwanda.
”Makubaliano
haya ni muhimu sana kwetu kwa sababu yataweza kuwasaidia vijana kuweza kuongeza
wigo wa kujiajiri lakini pia kuweza kutambua teknolojia za kisasa zinazotumika
katika viwandani kwa nyakati hizi ambazo teknolojia inakua siku hadi siku"
LEAH
DOTO LUKINDO Mkurugenzi VETA kanda ya Dar es salaam alisema makubaliano
yaliyofanyika baina ya kampuni ya SIKA pamoja na VETA yatakuwa na manufaa sana
kwa VETA hasa tunapoelekea kwenye uchumi wa Viwanda kwani ili kuwa na uchumi
imara lazima tuwe na vijana walio na ujuzi unaostaili.
Aidha
Mkurugenzi huyo aliongeza kwa kusema kuwa mojawapo ya njia ya kujenga ujuzi
unao hitajika kwa vijana ni vizuri kuweka ushirikiano kwa viwanda pamoja na
mashirika ambayo yatawasaidia wanafunzi wa VETA pamoja na walimu wake kujua
teknolojia inayotumika katika viwanda .
"
ushirikiano wa SIKA kama kiwanda kinachohusika na utengenezaji wa bidhaa za
ujenzi na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA utawasaidia vijana
wetu kupata fursa ya kujifunza matumizi ya bidhaa za ujenzi zinazozalishwa
katika kiwanda hicho kwani Matarajio ya VETA baada ya makubaliano haya ni
kuwasaida vijana kuweza kuajirika kwa urahisi na kuweza kujiajiri wenyewe
katika soko la Ajira."
Naye Mkuregenzi Mtendaji wa SIKA Tanzania ndugu ALFONSO PARADINAS alisema “tumeona ni muhimu kushirikiana na VETA ili kushiriki katika utoaji na uendelezaji wa elimu kwa kuwafundisha vijana teknolojia ya kisasa ambayo italeta manufaa kwao pindi watakapo ingia kwenye soko la ajira”
aliongeza
kwa kusema kuwa madhumuni ya kusaini makubalino hayo ni kuisaidia VETA kwa
kuwapatia wataalamu na kuwafundisha walimu wa VETA na baadae walimu hao
kuwafundisha wanafunzi wa chuo cha VETA Chang’ombe teknolojia mpya za kampuni
hiyo kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya kufundishia katika karakana za sekta ya
ujenzi.
Aliongeza
kwa kusema kwamba wao watatoa vifaa vya kufundishia katika karakana za Mafunzo
ya Ujenzi.
SIKA
Tanzania Construction Chemicals LTD ni tawi la kampuni ya Kimataifa ya SIKA
GLOBAL iliyoanzia USWIZI zaidi ya miaka 110 iliyopita, kampuni hii ina matawi
zaidi ya 100 duniani ikiwemo 18 katika bara la africa pekee. Nchini Tanzania
kampuni hii imeanza mwaka 2015 na imefanikiwa kufungua kiwanda cha uzalishaji
wa kemikali za aina zote zinazotumika kwenye zege (concrete mixture dio
admixture).
No comments:
Post a Comment