Mamlaka ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi VETA jana tarehe 12/03/2019 imetoa msaada wa mafuta maalumu ya
kuzuia madhara ya mionzi ya jua kwa watu
wenye ulemavu wa ngozi wanaotoka kituo cha
Albino Technical Service. Mafuta hayo yanasaidia watu wenye ualbino na
athari zinazotokana na mionzi ya jua ikiwemo pamoja na salatani ya ngozi.
Msaada huo umegharimu
zaidi ya shilingi laki nane.
Akikabidhi msaada huo
kwa miaba ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Bi. Rehema Binamungu ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi wa Utahini na Utunuku alisema, licha ya kuwa mafuta hayo hayawezi
kutosheleza mahitaji ya watu wenye ualbino kulingana na wingi wa uhitaji lakini
msaada huo ni ishara ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA
kuguswa na kundi hilo.
Bi. Binamungu
alitumia fursa hiyo kuwashauri watu wenye ulemavu kuhamasishana katika
kuangalia na kutumia fursa za mafunzo ya ufundi stadi ili kujiongezea ujuzi na kujikwamua kiuchumi.
“VETA tuna toa mafunzo ya aina mbalimbali
yanayo lenga mahitaji ya makundi ya watu mbalimbali hivyo tunafursa sawa kwa
kila mhitaji”
Kwa upande wake?
mwakilishi wa kikundi cha Albino Technical Service Bi. Anna Luhoga aliishukuru
VETA kwa msaada huo akisema kuwa wengi wa watu wenye ualbino hawana uwezo wa
kununua mafuta hayo kwa kuwa yana bei kubwa.
”tunaishukuru VETA
kwa kutupatia msaada huu kwa sababu mafuta haya yanauzwa kwa gharama kubwa na
wengi wetu tunashindwa kuyanunua.
Shughuli za watu wenye ulemavu wa ngozi
mara nyingi ni za mikono, hali inayowapelekea muda mwingi kushinda juani
hali inayosababisha kuharibika kwa ngozi
zao, ” alisema.
Aliiomba VETA
kuwasaidia watu wenye ulemavu katika masuala ya elimu ya ujasiriamali ili
waweze kuongeza ujuzi katika kuendesha shughuli za kujiongezea kipato.
No comments:
Post a Comment