Chuo
cha VETA Chang’ombe kimetoa msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya
sh. Milioni Moja katika Kambi ya Wazee Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Msaada
huo umetokana na mchango wa Wanawake wa chuo hicho katika kuadhimisha siku ya
wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila Machi 8 ya kila mwaka.
Akizungumza
na Wazee wa Kambi ya Nunge Kaimu Msajili wa Chuo cha VETA Chang’ombe Clara Kibodya
amesema kuwa wanawake wamekuwa na mwitikio katika kambi ya Nunge na hivyo
kuamua kutoa mchango wao kwa jamii inayoishi hapo.
Amesema
kuwa Kambi hiyo inahitaji msaada, na kutaka wadau na mtu mmoja moja kuona kuna
umuhimu wa kutoa msaada kwani serikali pekee yake haiwezi kutosheleza.
“Tumefika
na kujionea hali ya wazee na kuamini wanauhitaji wa msaada na tumevutiwa kama
wanawake ndio wasimamizi wa familia hatuwezi tukawaacha wazee hao kwani ni baba
zetu na babu zetu katika mila na tamaduni za Afrika”.amesema Kibodya.
Nae
Katibu Mukhtasi wa Chuo hicho Bena Maimu amesema katika kuadhimisha siku
wanawake duniani Kambi ya Nunge imewagusa na kutaka kuwa na utaratibu wa
kuwatembelea mara kwa mara na kujua changamoto zao ili wazee wasione jamii
imewatupa.
Kwa
upende wa Afisa Kilimo na Msimamizi wa Kambi ya Nunge Frank Munuo amesema kuwa
msaada huo ni mkubwa sana kwani kuna watu wana uwezo lakini hawajawahi kusaidia
kambi hiyo.
Amesema
kambi imepokea mssada kwa mikono miwili na kuwataka VETA kuwa mabalozi wa
kuwambia watu wengine katika kuwasaidia.
Akitoa
shukrani mmoja wa wazee wa Kambi ya Nunge Salum Ubwabwa amesema kuwa wanawake VETA
wamekuwa mstari wa mbele katika kuwajali hivyo waendelee kuwa na moyo huo huo
kuwakumbuka kwani wanauhitaji wa msaada.
No comments:
Post a Comment