Dkt.
Bujulu alisema hayo Septemba 7 alipokuwa akifunga rasmi warsha ya kuwajengea
uwezo makatibu muhtasi, makatibu waendesha ofisi, watunza kumbukumbu na
watumishi wa mapokezi juu ya uboreshaji huduma kwa
wateja iliyofanyika katika Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi (MVTTC), mkoani
Morogoro.
Alisema
wateja wanategemea kupata huduma bora kutoka kwa Mamlaka na wana haki ya
kuzipata kwa viwango bora.
Aliwataka
wafanyakazi wa VETA kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiendeleza kielimu ili
waweze kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika kada zao na kusisitiza kuwa
Mamlaka itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa fursa hizo kwa usawa kwa
wafanyakazi wake.
“Mnapopata
fursa za masomo sehemu mbalimbali tafadhali zichangamkieni kwa kuwa elimu
itawasaidia kuboresha utendaji wenu na hata kuwawezesha kukua katika muundo na
kupandishwa mishahara na vyeo”. Alisema.
Warsha
hiyo ilifanyika kwa siku mbili, tarehe 6 na 7 Septemba 2019 iliwajumuisha
makatibu muhtasi, makatibu waendesha ofisi, watunza kumbukumbu na watumishi wa
mapokezi 30 kutoka ofisi ya VETA Makao makuu, vyuo na ofisi za kanda.
Katika
warsha hiyo, mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo mbinu za Kuboresha Huduma kwa
Mteja, Uandaaji na Usimamizi wa Shughuli, Itifaki na kushirikishwa baadhi ya
miongozo iliyoandaliwa siku za karibuni ikiwemo Mkataba wa Huduma kwa Wateja na
Mwongozo juu ya Mwonekano wa Mamlaka (Branding Guidelines) inayolenga kuboresha
utoaji huduma kwa wateja.
No comments:
Post a Comment