CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Monday, 2 December 2019

Wahitimu VETA Waaswa Kujiajiri



Wahitimu wa vyuo vya Ufundi Stadi wameaswa kutumia vyema ujuzi walioupata kujiajiri wenyewe badala ya kusubiria kuajiriwa.


Akizungumza katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA Dar es Salaam Novemba 8, 2019 Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Kioo Limited Jacob Msuya amesema kuwa wahitimu wa VETA wana nafasi kubwa zaidi ya kujiajiri wenyewe kutokana na mafunzo kwa vitendo waliyoyapata kutoka vyuo vya VETA.
Msuya amesema kuwa anaamini mafunzo ya ufundi stadi yanawawezesha zaidi wahitimu kuwa na ueledi wa kufanya kazi kwa vitendo na kuwa wabunifu wa baadhi ya vitu mbalimbali vinavyohitajika kwenye jamii zao.
Aliwasifu wahitimu wa VETA akitolea mfano wa wahitimu anaofanya nao kazi katika kampuni ya Kioo na kusisitiza kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa weledi wa hali ya juu huku wakizingatia nidhamu.

“Ninategemea baada ya kutoka hapa watakwenda kuleta matokeo chanya ya taaluma walioipata kwa kufanya kazi kwa bidii na sio kuwa na cheti kisichokuwa na kazi ilhali kuna watu waliwekeza katika kuhakikisha vijana hawa wanapata ujuzi stahiki utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri wenyewe” Alisema


Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam Violeth Fumbo amesema jumla ya vijana 556 wamehitimu mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali  ambapo kazi yao kubwa ni kwenda kutumikia taifa kwa ujuzi walioupata.

Aliwataka wahitimu waende na mfumo wa kuanzisha vikundi ambapo wanaweza kuanzisha viwanda vidogo na taasisi za fedha kuwakopesha ili kuendeleza viwanda hivyo huku akiwasihi kujiendeleza zaidi kielimu.

Rais wa Serikali ya Wanafuzi wa chuo hicho Nurdin Chambalini amesema kuwa wahitimu wa VETA wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutekeleza sera ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda hivyo ni wajibu wao kuchangamkia fursa zilizopo.

No comments:

Post a Comment