Je
wewe ni Mbunifu wa Teknolojia au suala lolote la Kisayansi au Maarifa Asilia?
Karibu ushiriki katika Mashindano ya Kitaifa ya
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU).
Kuhusu MAKISATU: Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,
Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yameanzishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia kwa lengo la kutambua, kuendeleza na kubiasharisha
ubunifu katika sayansi na teknolojia ili kuchangia katika kufikia lengo la
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati
unaoendeshwa na viwanda.
Kaulimbiu na Kilele cha MAKISATU 2020: Mashindano hayo yanafanyika mwaka huu
yakiwa na Kaulimbiu, “Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi wa
Viwanda” na kilele chake kinatarajiwa
kufanyika Dodoma mwezi Machi.
Uratibu
wa VETA: Katika Mashindano
hayo, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inaratibu mchakato
wa mashindano katika ngazi ya Vyuo vya Ufundi Stadi na Sekta Isiyo Rasmi.
Shiriki mashindano: VETA inawakaribisha wabunifu wa
Teknolojia na masuala ya Kisayansi au Maarifa Asilia walio kwenye Vyuo vya
Ufundi Stadi au Sekta Isiyo Rasmi kushiriki mashindano hayo.
Mwisho wa
kuwasilisha fomu za maombi ni tarehe 31 Januari 2020. Pakua hapaMwongozo na Fomu kwa ajili ya Mashindano hayo.
Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi, piga
simu au tuma ujumbe kwenda 0736505027 au 0755267489 au Barua pepe pr@veta.go.tz
No comments:
Post a Comment